Ndoto ya golikipa namba mbili wa Manchester city Willy Cabarello ilionekana kutimia usiku wa jana baada ya mshambuliji hatari wa Monaco Radamel Falcao kutupia nyavuni bao 2.
Cabbarello alitoa tahadhari kwa walinzi wa timu hiyo kumchunga nyota huyo ambaye kwa sasa ameanza kurejea kwenye kiwango chake. Kama Falcao amefunga goli 19 kwenye mechi 25 alizocheza hakuna swali juu ya uwezo wake wa awali.
Si jambo la kushangaza kwa nyota huyu ambaye ni mkali wa kufumania nyavu ambaye aliwahi kuwa tishio katika ligi ya Hispania (La liga), Europa ligi hata klabu bingwa Ulaya wakati huo akiitumikia Atletico Madrid.
Licha ya Falcao kuandamwa na majeraha ambayo mara kadhaa yalimtoa kwenye ubora wake alipokuwa na Chelsea pamoja na Man utd lakini nyota huyo wa Colombia anawekwa katika kundi la washambuliaji bora kuwahi kutokea duniani.
Bila shaka wasifu wa Falcao ndiyo uliompa hofu golikipa wa Man city Willy Cabarello ambaye alitabiri kweli kwa mabaki wake. licha ya Monaco kupoteza mechi hiyo bado Falcao alionekana tishio na shujaa wa Monaco kama ilivyotabiriwa na kipa wao.

Comments
Post a Comment