Ibra atabeba taji na Man utd?


Mshambuliaji nyota wa Manchester united huenda akawa habari ya England kama man utd itatwaa taji la EFL katika uwanja wa Wembley leo.

Zlatan Ibrahimovic au maarufu kama Ibra Kadabra amewahi kuwa nyota kwenye klabu kadhaa ikiweo Juventus, Intermilan, AC Milan, Barcelona na PSG.

Kote huko Ibra amepita kwa mafanikio makubwa nadhani kwa watazamaji na wapenzi wa soka wanafahamu zaidi jambo hilo.

Ibra anahitaji mafaniko na Man utd?

Licha ya kuwa umri wake kufikia miaka 36 lakini kiwango chake kimezidi kuwa bora kila siku, nadhani ana kiu ya mafanikio ndani ya klabu hiyo bora duniani.

Siku chache wakati Ibra anatua Old Trafford Eric Cantona ambaye ni nyota wa zamani wa Man utd alimkaribisha nyota kwa kumwita Ibrahimovic mwana wa mfalme.

Hata hivyo Ibra alikata kauli ya mkongwe huyo wa Ufaransa baada ya kumjibu kwmba atakuwa mungu wa Man utd.

Kuitetea kauli ni lazma Ibra afanye vitendo halisi, ambapo kwa sasa ametupia goli ambazo hazipungui 30 tangu alipojiunga na Man utd.

Ni wazi kuwa ndoto ya Ibra ni kuingoza Man utd kubeba taji hilo jion ya leo katika uwanja wa Wembley, ili kumtambia kwa Vitendo.

Nina imani kuwa atacheka nyavu endapo hatopatwa masahibu ya ugonjwa au majeraha akacheza mchezo huo Leo.

Ni matumani yangu Ibra yupo kwenye mkakati mzito wa kuongeza mahaba ya mashabiki wa Man utd kwa upande wake, taji la leo ni muhimu kwa Ibrahimovic.

Ingawa mpira ni mchezo wa dakika 90 lakini kuna makubwa ya Ibra yanaweza kutokea Wembley jioni ya leo.

Comments