Beki wa kimataifa wa Uganda Juuko Murshid amerejea rasmi kwenye kikosi cha Simba.
Juuko alikuwa nchini Uganda tangu 'The Cranes' ilipoondolewa kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon January mwaka huu.
Ujio wa Murshed unaweza kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Simba kutokana na majeraha yanayomuandama Method Mwanjali.
Simba itashuka tena dimbani Machi 4 mwaka Huu katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Taifa.

Comments
Post a Comment