Simba sports leo imetoka kifua mbele baada ya kuikalisha Yanga kwa kipigo cha mabao 2-1.
Simba ilicheza pungufu kwa takribani dakika 30 kipindi cha pili lakini waliweza kuibuka na pointi za ushindi.
Yanga ndiyo iliyoanza kupata ushindi baada ya kupata bao la kuongoza kupitia Simon Msuva, hata hivyo Simba ilichomoa bao hilo kupitia Laudit Mavugo na kufunga la ushindi kupitia Shiza kichuya.
Simba imerejea kileleni rasmi ikiongoza kwa pointi 5 mbele ya mpinzani wake Yanga.

Comments
Post a Comment