Lallana ajipiga pini Liverpool hadi 2020


Kiungo wa Liverpool Adam Lallana amejifunga rasmi kwenye timu baada ya kusaini mkataba hadi mwaka 2020.

Kiungo huyo wa England anaingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi katika timu ya Liverpool ambapo kwa sasa atapokea kiasi cha £110000 kwa wiki nyuma ya Phelipe Coutinho anayepokea £150000.

Adam alitua Liverpool miaka 3 iliyopita akitokea Southampton kwa ada ya uhamisho wa £25 milioni.

Comments