Liverpool yajindaa kuachana na uwanja wao wa Mazoezi.


Uongozi wa timu ya Liverpool unajiandaa kutangaza kuachana na Melwood ambao ndiyo uwanja wao wa mazoezi.

Hatua hiyo imekuja kutokana umbali wa maili 5 ulipo kati ya Melwood na Kirby academy inayozalisha vijana wa timu hiyo.

Liverpool chini Jurgen Klopp imeandaa mpango mpya wa kuiweka karibu timu ya vijana dhidi ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mpango huo utaigharimu Liverpool kiasi kisichopungua £50 milioni.

Comments