Timu ya Manchester city imeanza vizuri katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuichapa Monaco 5-3.
Katika mechi hiyo Monaco ilitoka kifua mbele katika kipindi cha kwanza baada ya kuongoza kwa bao 2-1.
Hata hivyo Manchester city waliweza kurudi vizuri katika kipindi cha pili na kuiadhibu Monaco bao 4 kupitia Kun Aguero aliyefunga mara 2, John Stones na Leroy Sane.

Comments
Post a Comment