Timu ya Manchester united imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuitwanga St Etienne jumla ya mabao 4-0.
Katika mchezo wa kwanza Man utd ikiwa nyumbani iliilaza St Etienne kwa bao 3-0 kwa sifuri bao zote zikiwekwa nyavuni na Ibrahimovic.
Man utd imefunga hesabu ya goli 4-0 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Ufaransa.
Bao la pekee la ushindi la Man utd lilifungwa na Kiungo Henrink Mkhitaryan katika dakika ya 17 ya mechi hiyo.

Comments
Post a Comment