Manara: uzee unaitesa Yanga


Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa wachezaji wenye umri mkubwa ndiyo tatizo Yanga.

Manara alisema kikosi cha Simba kimesheeni vijana hali iliyowafanya Yanga kushindwa kumudu kasi yao kwa dakika 90.

"Tatizo la Yanga ni wachezaji wenye umri mkubwa, na hii imewashinda kucheza na Simba kwa dakika zote 90.

" Sisi tulishambulia na kuwachosha zaidi, na ndiyo maana tuliweza kutoka na matokeo ya ushindi." Alisema Manara

Baada ya ushindi dhidi ya Yanga Simba itashuka dimbani dhidi ya Mbeya city Machi 4 mwaka huu.

Comments