Baada ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba hatimaye baadhi ya mashabiki wameonekana kuchukizwa na ujio wa kocha wa sasa George Lwandamina.
Kitendo cha kuondolewa kwa Hans Pluijm ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa benchi la ufundi Yanga limekuwa kitendawili kwa mashabiki ambao wana imani kocha wa sasa ameiharibu Yanga.
Wapo mashabiki walioponda aina soka ambalo Yanga inasakata kwa sasa, wakiamini kasi kubwa imepungua ndani ya kikosi ni tofauti na ilivyokuwa chini ya Muholanzi huyo.
Pia wapo mashabiki wengine wanaoponda juu ya uwepo wa kiungo wa sasa Justice Zulu ambaye alitokea Zesco Muda mfupi baada ya kutua kocha wa sasa.
Lakini ukweli unabaki kuwa bado George Lwandamina anahitaji muda wa kutosha ili kuiweka sawa Yanga katika aina ya mfumo ambayo anategemea timu hiyo ndivyo itakavyocheza.
Mashabiki wa Yanga wanapaswa kuwa na utulivu ikiwa ni pamoja na kuisapoti timu yao iendelee kufanya vema katika mechi zifuatazo.
Hans Pluijm alifanya vizuri akiwa na Yanga kwa miaka miwili iliyopita na kuiburuza Simba akiondoka pointi 6 na Yanga ikatwaa ubingwa, wanayo haja ya kumbuka kocha huyo.
Nadhani wana nafasi ya kusahau yaliyopita na sasa wanatakiwa kuwa bega kwa bega na kocha wa sasa ambaye huenda siku za mbele mashabiki wakamkubuka zaidi kuliko Pluijm.

Comments
Post a Comment