Kiungo wa Arsenal Santi Carzola ataukosa msimu mzima wa ligi kuu kutokana na jeraha la enka linalomuandama.
Carzola hajacheza mechi yoyote tangu Arsenal ilipotoka na ushindi wa bao 6-0 dhidi Ludogorets ambapo alifanyiwa mabadiliko ya lazima.
Raia huyo wa Hispania mwenye miaka 32 ameifungia Arsenal mara mbili msimu huu, alifunga dhidi ya Watfrod mwezi wa nane mwaka jana na dhidi ya Southampton mwezi uliofatia.
Carzola alisajiliwa kutokea Malaga ya Hispania kwa dau la paundi 16 milioni mwaka 2012 na hadi sasa ameifungia Arsenal jumla ya magoli 29 katika mechi 189 alizoichezea timu hiyo.

Comments
Post a Comment