Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo amesema kuwa hatapunguza kasi yake ya kufunga uwanjani.
Mavugo ambaye amefunga kwenye michezo yote mitatu ya mwisho ana imani kubwa ya kuwafunga wapinzani wao Yanga watakapokutana jumamosi ya wiki hii.
"Nina imani na kiwango changu cha sasa, na nitaendelea kufunga magoli uwanjani, pia nina imani kubwa ya kuwafunga Yanga." Alisema Mavugo
Hivi karibuni nyota huyo aliyeibukia katika klabu ya Vital O' ya nchini Burundi amekuwa na kasi ya kufunga mabao na taratibu ameanza kurejea kwenye kiwango chake.

Comments
Post a Comment