Mourinho: Mnashangaa ya Pogba, makubwa yanakuja zaidi


Kocha wa Man utd Jose Mourinho amesema kuwa dau la Pogba litafunikwa hivi karibuni katika usajili wa majira ya joto.

Mreno huyo alisema kuwa Man utd inajiandaa kufanya usajili mkubwa katika kipindi cha majira ya joto ambapo dau la pogba litapigwa chini hivi karibuni.

Inasadikika kuwa Man utd itavunja benki ili kufanikisha usajili wa mshambuliaji Antonio Griezman anayekipiga katika klabu ya Atletico Madrid.

Kauli hiyo ya Mourinho ni kiashiria kuwa dili hilo limefikia pazuri na huenda Griezman akatua Old Trafford katika kipindi cha majira ya moto.

Comments