Beki wa Simba Method Mwanjali huenda akaikosa mechi dhidi ya Yanga Februari 25 mwaka huu.
Mwanjali alishindwa kumaliza mechi dhidi ya Prisons baada ya kukumbwa na majeraha ambapo alitolewa kwa machela katika dakika ya 62.
Chanzo kimeeleza kuwa hakuna asilimia mia moja kuwa huenda raia huyo wa Zimbabwe atakosa au kushiriki mechi hiyo.
"Bado ni mapema kuzungumzia, kuna muda mwingi kidogo kufikia mechi hiyo anaweza kuwepo au kukosa mechi hiyo." Kilisema chanzo.
Simba na Yanga zinakutana katika raundi inayofuata kwenye ligi kuu baada ya kucheza michezo 22 mpaka sasa.

Comments
Post a Comment