Kocha wa Newcastle Rafael Benitez amepata pigo baada ya kumkosa mfungaji wa timu Dwight Gayle kwa kipindi cha mwezi mmoja kutokana majeraha.
Gayle 25, ameifungia Newcastle mabao 20 pekee hadi sasa na ndiye kinara wa ufungaji mabao katika ligi hiyo.
Gayle alishindwa kumaliza mechi dhidi ya Aston Villa usiku wa jumatatu kutokana na tatizo la misuli kwenye nyama za paja.
Juhudi za Gayle zimeiwezesha Newcastle kuongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo hadi sasa inaongoza kwa pointi 69 ikifuatiwa na Brighton yenye pointi 68.

Comments
Post a Comment