Ngoma, Bossou wanaipotezea Yanga kiana


Nyota wawili wa Yanga Vicent Bossou na Donald Ngoma wanaonekana kuipotezea  Yanga kiaina kutokana na mgomo wao usioisha.

Bossou amegoma kurejea kwenye kikosi cha Yanga muda mrefu tangu kumalizika kwa michuano ya kombe la AFCON iliyofanyika nchini Gabon.

Bossou anadai mshahara wa miezi minne ambao bado hajalipwa na timu hiyo tangu mwaka jana.

Hali kadhalika ipo hivyo kwa Donald Ngoma ambaye anasadikika kuwa na jeraha la goti ambalo limesababisha asirejee kikosini kwa wakati kwenye kikosi cha Yanga.

Taarifa za chini chini zimebaini kuwa Ngoma anaikingia mgongo Yanga na hivyo ameweka mgomo baridi na kusingizia majeraha ikiwa bado hajalipwa mshahara wake.

Bossou ameweka wazi kuwa yuko tayari kutimka Yanga endapo watamlipa malipo yake anayowadai kwa miezi minne.

Bila shaka Ngoma na Bossou wanaipotezea Yanga kiaina huenda wameona kuna maisha ya ujanja ujanja na kukosekana kwa heshima kwenye malipo.

Kuna haja ya kujua tofauti ya wachezaji wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania. Aina ya wachezaji kama Ngoma na Bossou hawataki kupelekeshwa na kuburuzwa na ujanja ujanja wa Tanzania.

Kwa mtazamo wangu ni kuwa Bossou na Ngoma wanajiamini kutokana na uwezo wao wa kusakata kabumbu na ndiyo maana wanajua Yanga inawahitaji.

Licha ya Yanga kuwahitaji lakini pia wanaamini kupata klabu bora na kwa malipo mazuri ndani ya Africa na nje ya Africa.

Nadhani wanaipotezea Yanga kiaina nadhani hawana mipango ya kuendelea na soka la Tanzania na ndiyo maana wanaonekana kuamini misimamo yao binafsi.

Comments