Kiuongo na nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima ameisifu Simba kwa kiwango kizuri ilichokionesha.
Niyonzima alizungumza maneno hayo baada ya filimbi ya mwisho iliyohitimisha dakika 90 za mchezo huo hapo jana.
"Simba wanastahili pongezi, licha ya kuwa pungufu walituzidi uwezo, walicheza vizuri na wamestahili ushindi." Alisema Niyonzima
Shiza Kichuya ndiye aliyeibuka Shujaa kwenye mechi hiyo baada ya kuipatia Simba bao la ushindi katika dakika ya 80 ya mechi hiyo.

Comments
Post a Comment