Payet, Depay waanza vizuri Ufaransa


Waliokuwa nyota wa ligi ya England Dimitri Payet pamoja Memphis Depay wameanza vizuri kwenye ligi ya Ufaransa baada ya kuzifungia klabu zao mpya.

Payet amerejea Mersaille baada ya kuitumikia West Ham kwa misimu 2, na Memphis Depay ametua Olympic Lyon.

Wote kwa pamoja walifungia timu zao, Payet aliiongoza Mersaille katika ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Guingamp na Memphis aliifungia Lyon katika ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Nancy.

Memphis alishindwa kuwika katika timu ya Man utd tangu aliposajiliwa mwaka mmoja uliopita akitokea PSV ya Uholanzi.

Comments