Baada ya kuiongoza Leicester city kwenye ubingwa msimu uliopita hatimaye Claudio Ranieri ameondolewa kwenye timu hiyo.
Ni miezi tisa pekee imepita hadi sasa tangu Ranieri apitie Leicester city ubingwa wa ligi kuu, na sasa ameondolewa rasmi.
Leicester haijafanya vizuri msimu huu ambapo hadi sasa inashika nafasi ya nne kutoka mwisho ikipigana isishuke daraja.
Hofu ya kushuka daraja ilitawala kwa mabosi wa timu na hivyo wameamua kumwondoa Raia huyo wa Italy.

Comments
Post a Comment