Mshambuliaji wa Manchester united Wayne Rooney amesema kuwa ataendelea kubaki Old Trafford licha ya kupokea ofa nyingi kutoka China.
Baadhi ya timu kadhaa katika ligi ya China wakiwemo mabingwa ligi hiyo Guangzhou Evergrande inayonolewa na Felipe Scolari pamoja na Beijing Guoan ambayo ilishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi zinataka kumfanya Rooney kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani.
Licha ya kupokea ofa nono kwenye klabu hizo, Rooney aliyebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake amekataa kupokea mabilioni ya wachina hao.
Rooney 31, alikuwa moja kati ya wachezaji walioungana na Jose Mourinho katika maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi katika kipindi cha majira ya joto mwaka jana.

Comments
Post a Comment