Timu ya Simba leo itashuka dimbani katika mchuano wa kombe la shirikisho dhidi ya African Lyon katika uwanja taifa jijijni Dar es Salaam.
Simba inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi ya mwisho waliocheza dhidi ya African Lyon walipolala kwa bao 1-0.
Kwa pamoja Simba na Lyon zina kibarua kizito cha kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ikiwa ni nafasi pekee kwa timu hizo endapo mmoja wapo atatumia nafasi hiyo ipasavyo.
Soka ni mchezo was dakika 90, si Simba wala African Lyon ambayo inapewa asilimia 100 ya kutinga robo fainali kwa kuwa ni dhahiri kuwa matokeo ya mpira ni matatu.
Simba chini ya safu ya ushambuliaji ambayo inaundwa na Juma Liuizio, Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo imeanza kuwa tishio hivyo ngome ya African Lyon ambayo inaongozwa na Hassan Isihaka inatakiwa kujipanga ipasavyo.
Ingawa kwa mtazamo unaweza kuhisi Simba ni pekee mwenye nafasi ya hiyo kutoka na kujeruhiwa na Lyon, lakini kwa upande Lyon nao wapo kwenye kiwango bora hivyo Simba nao wana kibarua kigumu.
Mechi ya leo itakuwa na utamu wa aina yake huku matarajio ya wana Simba yakiwa ni kuwaondoa Lyon mashindanoni na kulipa kisasi kwa kile walichokifanya kwenye mechi ya kwanza.

Comments
Post a Comment