Simba, Yanga nani kuibuka mbabe leo?


Simba na Yanga zitashuka dimbani leo kutafuta nani atakayeibuka mbabe na kuzoa pointi 3 katika raundi ya pili ya ligi hii.

Katika mechi ya kwanza timu zote zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 hadi mwisho wa kipenga cha mwamuzi Martin Saanya.

Simba inaongoza ligi kwa muda baada ya kuzoa ikiwa na pointi 45 ikifuatiwa na Yanga yenye 43 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Yanga imetwaa ubingwa mara 2 mfululizo inataka kutete taji hilo kwa mara ya tatu. Simba inataka kufuta ukame wa ubingwa ikiwa na misimu 4 haijanyanyua taji hilo tangu mwaka 2012.

Ushindani ni mkubwa baina ya timu hizo mbili. Yanga inanonekana kuwa hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji na Simba ikitamba kwenye kiungo.

Kombinesheni ya Yanga inayoundwa na Simon Msuva, Deus Kaseke na Amis Tambwe ndiyo iliyozaa mabao mengi zaidi ligi kuu.

Simba imeonesha kuiva kwenye safu ya kiungo, ambapo ndiyo klabu iliyoruhusu mabao machache zaidi msimu huu.

Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo anaonekana kurudi kwenye kiwango chake hadi sasa. Tangu kocha Joseph Omog alipoanza kuwatumia Ibrahim Ajibu, Juma Luizio na Laudit Mavugo safu ya ushambuliaji Simba imeonekana kuwa tishio.

Ni mchezo wa aina yake kati ya Simba na Yanga Siku ya leo, Nadhani yeyote ana nafasi ya kutoka na pointi 3.

Comments