'The special one' kupewa miaka 5 Man utd


Uongozi wa Manchester united upo kwenye mchakato wa kumuongeza Jose Mourinho miaka mitano ya kuinoa timu hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na mabadiliko makubwa yaliyojitokeza kwenye timu hiyo tangu alipotua kocha huyo.

Tangu kutua kwa Mourinho kwa wababe hao wa England, wametengeneza mpunga mrefu kiasi cha £1 bilioni ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya timu hiyo.

Mourinho alibadili taswira ya timu hiyo baada ya kusajili nyota kadhaa akiwemo Zlatan Ibrahimovic, Paul Pogba, Henrikh Mkhitryan na Eric Baily.

Comments