Tetesi: Chelsea yatia mkono kwa Aguero


Timu ya Chelsea imejipanga kuweka mezani dau £75 milioni ili kuinasa saini ya Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero.

Chelsea inajipanga kusajili mfungaji bora zaidi kutokana na kusua kusua kwa mshambuliaji wa sasa Diego Costa ambaye huendea akatimka kwenye timu hiyo.

Vinara hao wanaokimbiza kwenye msimamo wa ligi kuu msimu huu wamekuwa kwenye wakati mzuri tangu kocha Antonio Conte atue kwenye timu hiyo.

Licha ya Sergio Aguero kuingia majeruhi mara kadhaa lakini kiwango chake bado kipo kwenye ubora na amekuwa mtaalamu wa kufumania nyavu mara zote.

Comments