Kocha wa Chelsea Antonio Conte anajipanga kumsajili Romeo Lukaku kutoka Everton msimu ujao.
Lukaku amezidi kuwa tishio tangu alipoachana na Chelsea na kutua Everton ambapo hadi sasa ametupia nyavuni goli 16 ambazo amefunga kwenye ligi kuu pekee kwa msimu huu.
Conte anataka kumrejesha Lukaku Chelsea ili kuongeza nguvu kwenye mapambano ya ushindani katika msimu ufuatao.
Hadi sasa Chelsea haijafikia mwafaka rasmi na mshambuliaji wa timu hiyo Diego Costa hali inayompelekea Conte kufikia maamuzi hayo.
Lukaku amewahi kuwa katika kikosi cha Chelsea lakini alishindwa kutamba chini ya Andre Villas Boas pamoja na Jose Mourinho.

Comments
Post a Comment