Usajili: Nyota wa Napoli kutua Arsenal.


Timu ya Arsenal inajipanga kuanza na usajili wa mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne.

Insigne mwenye miaka 25, ametikisa nyavu mara 8 tangu kuanza kwa msimu katika ligi ya Serie A.

Bado klabu ya Arsenal inakosa mshambuliaji wa uhakika atayeingoza timu kurejesha heshima yake ya awali katika mapambano ya ligi kuu pamoja na ile klabu bingwa Ulaya.

Hivi karibuni Arsenal iliangukia pua kwa Bayern Munich baada ya kukubali kichapo cha mabao 5-1 katika ligi ya mabingwa.

Comments