Usajili: Spurs yahamia kwa Martial


Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kufanya mpango wa kumsajili Antony Martial kutoka Man united.

Pochettino ambaye ni raia wa Argentina, yupo kwenye mipango kabambe ya kuijenga Spurs ambayo italeta ushindani zaidi kwenye ligi ya EPL pamoja na ligi ya mabingwa.

Martial amepoteza furaha ya awali tangu kutua kwa kocha Jose Mourinho kwenye timu hiyo.

Ujio wa Henrikh Mkhitaryan, Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba umemuweka kwenye wakati mgumu nyota huyo ambaye amepoteza namba kwenye kikosi cha kwanza.

Comments