Timu ya Real Madrid jana imeangukia pua katika mchezo wa ligi dhidi ya Valencia baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1.
Valencia ilipata mabao ya ushindi katika dakika ya 2 na ya 9 yakiwekwa nyavuni na Simon Zaza pamoja Orrelana na bao pekee la Real Madrid lilifungwa na nyota wa timu hiyo Christiano Ronaldo.
Matokeo hayo yameipa nafuu Barcelona ambayo inawafukuzia kwa pointi moja vinara hao wa Santiago Bernabeu wenye pointi 52 na mchezo mmoja mkononi.

Comments
Post a Comment