Baada ya kukaa nje ya uwanjani kwa takribani wiki tatu hatimaye Wayne Rooney arejea mazoezini.
Rooney alikuwa nje uwanja tangu February 1 mwaka huu kutokana na tatizo dogo la misuli kama ilivyoelezwa awali na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.
Man utd itashuka dimbani kesho kuivaa St Etienne katika raundi ya 32 ya Europa ligi katika mechi ya marudiano.
Licha ya Rooney kurejea uwanjani, Man utd itawakosa kiungo Ander Herrera pamoja Phil Jones ambaye anasumbuliwa na majeraha.

Comments
Post a Comment