Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa bado ana miaka minne mbele ya kuendelea kufundisha soka.
Raia huyo wa ufaransa alisema kuwa hakuna mahala sahihi kama Arsenal na huenda akaendelea kuwanoa washika bunduki hao.
"Nadhani Arsenal ndiyo mahala sahihi, nitaendelea kuwa mwalimu soka kwa miaka minne mbele.
" Bado nina nafasi hiyo, kati ya mwezi wa tatu au wanne nitaamua hatma yangu." alisema Wenger.
Arsene Wenger atamaliza mkataba wake na timu hiyo mwisho wa msimu huu endapo hatosaini kwa mara nyingine kuendelea na timu hiyo.

Comments
Post a Comment