Aggrey Morris arejea mazoezini


Beki kisiki wa timu ya Azam Aggrey Morris amerejea mazoezini baada ya kupona majeraha yake.

Morris aliumia sehemu ya mfupa wa paja katika mchezo wa kwanza ambao Azam ilikipiga dhidi Mbabane Swallows katika uwanja wa chamanzi.

Awali Morris alianza na mazoezi binafsi katika gym ya timu hiyo na jioni ya jana ameungana na wenzake katika mazoezi.

Azam itashuka itashuka dimbani jumamosi hii katika mtanange mkali wa ligi kuu dhidi ya Yanga SC katika uwanja wa taifa.

Comments