Ajib, Samatta kuongoza mashambulizi Stars.


March 25, 2017

Mshambuliaji wa KRC Genk Mbwana Samatta pamoja na Ibrahim Ajib wa Simba ndiyo watakao ongoza safu ya ushambuliaji katika kikosi cha Taifa Stars kitakachoshuka dimbani dhidi Ya Botswana leo.

Hii ni mechi ya kwanza kwa kocha Salum Mayanga ambaye amekabidhiwa jukumu la kuinoa Taifa Stars, tangu Bonifas Mkwasa alipoachana na timu hiyo.

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa kioo na msaada kwa kocha Salum Mayanga ambaye ameadhimia kuunda safu bora ya ushambuliaji.

Taarifa za awali zilithibitisha kuwa Mshambuliaji Thomas Ulimwengu hakuwa vizuri kiafya kwa ajili ya kuungana na kikosi hicho hali iliyopelekea kocha huyo kutengeneza kombinesheni ya Ajib na Samatta.

Wachezaji wa Taifa stars akiwemo nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta wamesifu ubora na mbinu za kocha huyo ambaye amewahi kuzinoa timu kadhaa zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Mbali na Taifa Stars Mayanga amewahi kuwa kocha wa Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya.

Comments