Aliyeitesa Simba mbioni kutua Yanga


Uongozi wa Yanga SC umetuma rasmi maombi ya kumsajili kiungo wa Mbeya City Kane Ally.

Nahodha huyo wa Mbeya city ndiye aliyeitesa Simba katika mechi ya mwisho ya ligi kuu ambapo simba ililazimisha sare ya bao 2-2 katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Kane Ally aliweza kuwadhibiti vilivyo viungo wa Simba akiwemo Jonas Mkude ambaye aliishiwa ujanja katikati.

Kutokana na tatizo la kiungo ambalo linaikabili Yanga kwa sasa wameamua kuandaa ofa rasmi kwa ajili ya kuinasa saini ya jembe hilo.

Hayo yamethibishwa na katibu mkuu wa Yanga Bonifas Mkwasa ambaye aliweka wazi kuanza kwa taratibu za kumnasa mbaya hiyo Simba SC.

Comments