Allegri atupilia mbali taarifa za kumrithi Wenger


Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri amekanusha uwepo wa taarifa ya yeye kuchukua nafasi ya Arsene Wenger.

Allegri alizungumza hayo muda mfupi baada ya kumaliza kwa mechi ya Udinese dhidi ya Juventus ambao walitoka sare ya bao 1-1.

"Arsenal hawajanipa taarifa hizo, bado mimi ni kocha wa Juventus na Wenger ni kocha wa Arsenal.

" Muda huwa unaamua kila kitu lakini kwa sasa naingalia Juventus ili tuweze kutetea taji letu." Alisema Allegri.

Comments