Alonso atangaza kuachana na soka.


Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Bayern Munich ya Ujermani Xabi Alonso ametangaza kustaafu soka mwisho wa msimu huu.

Alonso 35, amethibitisha taarifa zilizokuwa zimezagaa kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita baada ya kuandika kwenye kurasa zake za mitandao ya jamii kuhusiana na kustaafu soka.

Alonso alianza kuwika katika soka alipokuwa na klabu ya Real Sociedad ya Hispania, mwaka 2004 alitua Liverpool hadi 2009 ambapo alirejea La liga na kujinga na Real Madrid na mwaka juzi alitua Bayern Munich.

Comments