Arsenal kukipiga tena na Bayern Munich


Timu ya Arsenal imetangaza rasmi kucheza na Bayern Munich ikiwa ni sehemu ya utangulizi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi 2017/18.

Arsenal itacheza na Bayern Munich katika jiji la Shanghai China ikiwa ni moja ya mchezo wa kupima nguvu vikosi vyao.

Washika bunduki hao wa London watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 10-2 katika mchezo wa nyumbani na ugenini kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Comments