Uongozi wa Arsenal umekanusha kuwepo kwa taarifa za kufanya mazungumzo na Kocha wa Dortmund Thomas Tuchel.
Hadi kufikia jana taarifa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo viliripoti kuwepo kwa mazungumzo baina ya Arsenal na kocha huyo.
Hata hivyo uongozi huo umethibitisha kuwa hawajafikia mkakati wa kusaka kocha mpya atakayerithi nafasi ya Arsene Wenger ambaye anapingwa vikali na mashabiki wa timu hiyo.
Tuchel wenye miaka 43 amewahi kuzinoa FC Augsburg, Mainz 05 na sasa Dortmund ambayo ameiwezesha kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Comments
Post a Comment