Timu ya Azam imeanza rasmi mazoezi ili kujiandaa na mechi ya ushindani dhidi ya Yanga SC itakayopigwa April Mosi mwaka huu.
Mabingwa hao wa kombe la mapinduzi walipumzika kwa siku baada ya kurejea nchini ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa na Mbabane Swallows kwenye raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Azam imeanza mazoezi ikiwakosa nyota wake kadhaa ambao wanaunda kikosi cha timu ya taifa akiwemo Aishi Manula, Shomali Kapombe na Gadiel Michael kwa Upande wa Ulinzi.
Pia Azam inawakosa viungo wake Himid Mao 'Ninja', Frank Domayo na Salum Abubakar maarufu kama sure Boy.

Comments
Post a Comment