Baada ya kuong'olewa na Mbabane Swallows kwenye kombe la Shirikisho hatimaye Azam yaongeza nguvu kwenye ligi kuu na kombe la FA.
Azam inayonolewa na kocha Aristica Cioaba iliondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha bao 3-1 katika mechi ya nyumbani na ugenini dhidi ya Swallows.
Licha ya kutolewa kwenye michuano hiyo kocha wa Azam alisema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika ligi ya Vodacom na FA.
"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye ligi ya nyumbani, na nguvu zote tumehashia kwenye ligi hizi.
"Tunajipanga kufanya vizuri kwenye robo fainali ya kombe la FA lakini tuna kibarua kizito cha kujiweka pazuri kwenye ligi ya Vodacom." Alisema Cioaba.
Source: www.azam.co.tz

Comments
Post a Comment