Timu ya Barcelona imepigwa faini ya kiasi cha £16000 kutokana na tabia ziliooneshwa na mashabiki wake walipokutana na PSG.
Mashabiki wa Barcelona walihusika na kitendo cha kuingia uwanjani wakati timu hiyo ilipofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada kuifunga PSG bao 6-1.
Pia UEFA imeitoza faini ya kiasi cha £43000 timu ya St Etienne baada ya mashabiki wake kuwasha fataki uwanjani walipokutana na Man utd kwenye raundi ya 32 Europa league.

Comments
Post a Comment