Conte aweka mezani majina ya usajili.


Kocha wa Chelsea Antonio Conte amemkabidhi tajiri wa Chelsea Roman Abromovic majina ya wachezaji atakaosajili mwishoni mwa msimu.

Katika orodha hiyo yumo Alexis Sanchez wa Arsenal, Ryan Bertrand (Southampton) na Romelu Lukaku (Everton) ambao wote wote kwa pamoja waliwahi kuwa Chelsea.

Pia kocha huyo anahusishwa katika usajili wa beki anayefanya vizuri kwa sasa katika ligi ya England Michael Keane ambaye anakipiga katika timu ya Burnley.

Comments