Conte kuingia mkataba mpya na Chelsea


Kocha wa Chelsea Antonio Conte atarajiwa kufanya makubaliano ya kuboresha mkataba wake na timu ya Chelsea.

Raia huyo wa Italy alisaini miaka 3 hapo awali alipokuwa akitua Stamford Bridge hapo mwaka jana kipindi cha kiangazi.

Imeelezwa kuwa Chelsea inataka kumlinda kocha huyo ambaye ameanza kumezewa mate na klabu kadhaa barani Ulaya na China.

Mkataba mpya utamfanya Conte adumu zaidi kwenye timu hiyo na kuwa moja ya makocha ambao wanalipwa vizuri duniani.

Comments