Mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu jana alicheza kwa dakika 30 katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kufanyiwa mabiliko katika uwanja wa Jamuhuri.
Majeraha yalimuweka nje Busungu kwa muda mrefu hali ambayo imepelekea kushusha kiwango chake kwa asilimia 40%.
Ni wazi Busungu anastahili kutokea benchi, kwa kuwa amepoteza uwezo na kasi yake ya awali, benchi linaweza kuwa mahala pake wakati anatarajiwa kupandisha uwezo wake taraibu kama ilivyokuwa hapo awali.
Busungu alitolewa katika dakika 30 ya mchezo na nafasi yake ilichukuliwa na Juma Mahadh.
Obrey Chirwa na Amis Tambwe wanastahili kwanza, endapo Yanga itapata matokeo anaweza kutumia dakika 20 au 15 za mwisho kujiweka sawa.
Kuuguza majeraha kwa muda mrefu nadhani kulimfanya Busungu kustahili kucheza kwa dakika 30 dhidi ya Mtibwa Sugar hapo jana.

Comments
Post a Comment