Diego Costa atupia bao, Spain ikiua 4-1.

March 25, 2017

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga magoli katika ushindi wa Spain dhidi ya Israel.

Katika mechi hiyo Kiungo wa Manchester city David Silva ndiye aliyeanza kuona nyavu za Israel kwenye dakika ya 15, Vitolo dakika 45, Diego Costa dakika ya 51 na Isco dakika ya 88.

Diego Costa amefunga jumla ya goli 4 katika mechi nne za mwisho ambazo ameichezea Spain.

Comments