Griezman: sitaondoka Atletico


Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amesema kuwa hataondoka kwenye timu hiyo kama inavyohusishwa kwenye vyombo vya habari.

Griezmann mwenye miaka 25, amekuwa akihusishwa na Manchester United ambayo inataka kuandaa dau nono ili kukamilisha usajili wa mfaransa huyo.

Habari zilizokuwa zimezagaa mitandaoni zilieza kuwa huenda Man utd ikavunja rekodi ya dau la usajili wa Pogba kufikia £100 m ili Griezmann atue Old Trafford.

Licha ya Man utd fowadi huyo amekuwa akifukuziwa na baadhi ya timu kubwa barani Ulaya ikiwemo Chelsea, Barcelona na PSG.

Comments