Huyu ndiye mrithi wa Hazard Chelsea.


Kocha wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez endapo Eden Hazard atatimka Real Madrid.

Real Madrid inataka kuweka fungu nono linalokadiriwa kufikia £77 milioni kwa ajili ya kumnasa nyota staa huyo wa Ubelgiji anayefanya vizuri na kutamba katika ligi ya England.

Conte aliweka hisia zake wazi kuwa Alexis Sanchez ndiye mrithi Sahihi wa Eden Hazard ambaye anatabiriwa kutua Santiago Bernabeu kwenye dirisha kubwa la usajili.

Comments