Beki wa Simba Novaty Lufunga yuko nje ya kikosi cha Simba kilichopiga kambi kwenye moja ya hotel katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Lufunga atalazimika kukosa mechi ya Mbeya city kutokana na kadi tatu za njano ambapo kuingia uwanjani ni kinyume na kanuni za ligi kuu.
Lufunga alioneshwa kadi ya njano katika pambano dhidi ya Yanga baada ya kumshika Obrey Chirwa aliyekuwa mbioni kufunga goli.
Hata hivyo Simba itakuwa na Juuko Murshid ambaye hivi karibuni alirejea kwenye kikosi baada ya kukosekana kwa takribani mwezi mmoja.

Comments
Post a Comment