Kocha amtaka Toure Ivory Coast


Kocha wa mpya wa Ivory Coast Marc Wilmot amesema kuwa anamuhitaji kwa mara nyingine kiungo wa Manchester city Yaya Youre kwenye timu hiyo.

Wilmot alizungumza hayo baada ya kusaini mkataba wa miaka 2 wa kuinoa Ivory Coast alipokuwa jijini Abjan kwenye nchi hiyo.

"Nimemuona katika mechi mbili alizocheza mara ya mwisho Man city kwenye nafasi ya kiungo mkabaji bado yuko na ana nguvu za kutosha.

"Nitakwenda kumuona ili nifanye nae mazungumzo kwa ajili ya kumrejesha tena kwenye timu ya taifa." Alisema Wilmot

Wilmot 43, amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji ambapo aliingoza timu hiyo kwenye michuano ya UEFA Euro iliyofanyika Ufaransa mwezi Juni mwaka jana.

Comments