Liverpool yaitwanga Arsenal 3-1.


Timu ya Liverpool imeendelea kumweka kocha Arsene Wenger kwenye wakati mguu baada ya kuichapa Arsenal bao 3-1 katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ilifungu mabao hayo kupitia Roberto Firmino, Sadio Mane na Giorginio Wijnuldum na lile la Arsenal liliwekwa nyavuni na Danny Welbeck.

Kipigo hicho kinazidi kumweka mahala pagumu kocha Arsenal ambaye inasadikika huu utakuwa msimu wake wa mwisho kuwanoa washika bunduki hao wa London.

Comments