Lukaku agomea mkataba mpya Everton


Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku amegoma kusaini dili jipya na klabu hiyo.

Everton imeandaa mkataba mpya wenye lengo la kumlipa fowadi huyo £100,000 kwa wiki endapo atasaini dili jipya.

Licha ya ofa nono ambayo Everton imeandaa kwa ajili ya Lukaku kuna uwezekano Chelsea ikatibua dili hilo.

Kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte anavutiwa na mpango wa kumrejesha Lukaku katika uwanja wa Stamford Bridge ili Kuziba nafasi itakayoachwa wazi na Diego Costa.

Comments